Pages

Tuesday, December 18, 2012

UONGOZI WA SIMBA WATUMIA PESA ZA UHAI KULIPIA GYM NA KUACHA TIMU B IKITAABIKA

Baada ya kuvumilia kwa muda mrefu vitendo vya uongozi wa klabu ya Simba kutowapa huduma muhimu katika kuendesha timu ya B ya klabu hiyo, leo hii wachezaji na makocha wa timu Selemani Matola na Patrick Rweyemamu inasemekana wameamua kutoingiza timu hiyo uwanjani katika mchezo wa robo fainali ya kombe la Uhai linaloendelea katika viwanja vya Karume na Chamazi jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kilicho karibu na timu hiyo ya Simba B kimesema uongozi wa klabu hiyo umekuwa ukiwatelekeza wachezaji wa timu hiyo kwa muda mrefu katika kuwapa mahitaji yao ya kimsingi - "Kiukweli uongozi hauna habari hata kidogo na hii timu B, wamewaachia Matola na Rweyemamu kila kitu. Wachezaji wanadai mishahara ya miezi mitatu sasa, fedha zao za ushindi wa Kombe la BancABC hawakuambulia kitu chochote. Na juzi zile fedha za maandalizi walizotoa wadhamini wa Uhai Cup, wamechukua na kwenda kulipia gym kwa ajili ya timu A huku wakishindwa kutoa hata senti tano kwa ajili ya timu husika yenye kushiriki kombe la Uhai Cup ambayo ni timu B.

"Hii ni makusudi wanayofanya uongozi sio kwamba timu haina fedha, mfano angalia jzui wametoa $40,000 na mshahara wa $2000 kwa kipa Dhaira, pia wamempa Okwi mapesa kibao lakini wanashindwa kuangalia msingi wa maendeleo ya Simba SC ambao ni timu ya pili. Rweyemamu amekuwa akijitoa sana katika kuisadia hii timu ya pili lakini sasa anashindwa kuendelea kwa sababu uongozi hauonyeshi kuwa na mapenzi ya dhati na Simba B. Timu jana ilipata aibu kubwa wakati ikitoka Chamazi - basi walilokuwa wakitembelea liliishiwa na mafuta na kupaki barabarani, hivi kweli jambo kama hilo la kuitokea timu kubwa kama ya Simba kweli? Sasa kutokana na mambo yote hayo leo hii wachezaji wanataka kugoma kwenda uwanjani kesho ili kuushinikiza uongozi kutimiza mahitaji yao." - kilimaliza chanzo cha habari.

Kwa mtindo huu soka la Bongo litaendelea kudumaa mpaka tutakapopata viongozi wenye mapenzi na nia ya dhati ya kutaka maendeleo ya soka Tanzania

No comments:

Post a Comment