Pages

Sunday, December 2, 2012

NDOTO ZA SERENGETI BOYS ZAYEYUKA RASMI




NDOTO za kushiriki fainali za vijana waliochini ya miaka 17 ilizokuwa nazo timu ya taifa ya vijana waliochini ya miaka 17 "Serengeti Boys", zilizimika ghafla jana baada ya kufungwa mabao 2-0 na Congo Brazaville ugenini.

Serengeti boys ilitolewa rasmi kwenye hatua ya mwisho na vijana wenzao wa Congo Brazaville kwa jumla ya mabao 2-1 waliloshinda nyumbani wiki mbili zilizopita.

Kabla ya mchezo huu wa marudiano Serengeti ilikuwa ikihitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili kuweza kufuzu

Vijana hao ambao walikabidhiwa bendera ya taifa na mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa, Peter Tino walikuwa na ari ya kushinda mchezo huo japo walitaadharishwa ugenini wanaweza kufanyiawa mbinu chafu hivyo wao wafikirie mchezo tu.

"Nyie ni jeshi la Tanzania linalokwenda vitani ndio maana mmekabidhiwa bendera ya taifa hivyo mkapigane vema ila mjue kwenye mpira kuna machezo mchafu mbaeza mkakalishwa uwanja wa ndege muda mrefu ila nyie msijali fikirieni mchezo tu", aliwaasa Peter Tino wakati wakiondoka.

Maneno ya Tino hayakuwa ya bure kwani taarifa ambazo tulizipata zinasema kulikuwepo na mazingira ya vurugu zilizo andaliwa na wenyeji za makusudi kabla ya mchezo na hata wakati wa mchezo ambazo ziliwaathiri wachezaji wa Serengeti ikiwemo kupigwa na askari wa jeshi la polisi kwa kocha msaidizi  Jamhuri Kihwelu "Julio" na meneja wa timu, kipigo ambacho haikujulikana mara moja kilitokana na nini.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Angetile Oseah amesema walikuwa wakiwasiliana na viongozi walioambatana na kikosi hicho ili kujua nini kilitokea kabla, wakati wa mchezo na baada ya mchezo ndipo atakapoweza kutoa taarifa kwa umma.


Serengeti boys walifika kucheza hatua ya tatu baada ya raundi ya kwanza nchi ya Kenya kujitoa na raundi ya pili Misri kujitoa pia.

Tanzania haijaweza kupata tiketi ya kucheza fainali zozote za Afrika tangu mwaka 1980.





No comments:

Post a Comment