Pages

Friday, December 14, 2012

MVUA YASABABISHA MCHEZO KULALA

MVUA kubwa ilionyesha jana mkoani Iringa imesababisha mchezo wa Mshindo na Mtwa wa ligi daraja la nne kutomalizika.

Mvua hiyo ilianza kunyeshwa kipindi cha pili dakika ya 75 na kusababisha uwanja kujaa maji na kumlazimu mwamuzi kuhahirisha mchezo.

Mpaka mchezo unaahirishwa Mshindo walikuwa wanaongoza kwa mabao 3-0, yaliyofungwa na Francis Msovela dakika ya pili na 42 na Hassan Nyangaduke dakika ya 72.

Kufuatana na marekebisho ya kanuni za shirikisho la soka nchini, (TFF) mchezo huo utamaliziwa kwa muda uliobaki na matokeo yataendelea kama yalivyokuwa awali.

Akizungumza kwa njia ya simu toka Iringa Katibu Mkuu wa chama cha soka manispaa ya Iringa, Rashid Shungu alisema mchezo ulikuwa unaendelea vema ila ulishindikana kumalizika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo.

"Mchezo ulikuwa unaendelea vizuri lakini ghafla dakika ya 70 mvua kubwa ilinyesha na kusababisha uwanja kujaa maji na kufanya mchezo kushindwa kuendelea hivyo utamaliziwa muda uliobaki", alisema Shungu

No comments:

Post a Comment