Pages

Thursday, December 6, 2012

MICHEZO YA NUSU FAINALI YA CECAFA LEO MTOTO ATUMWI DUKANI


 
Patashika nguo kuchanika ya michuano ya Tusker Challenge cup inatarajia kuendelea tena jioni ya leo kwa michezo miwili ya nusu fainali ya michuano kupigwa katika dimba la Namboole nchini Uganda.
Mchezo wa kwanza utakuwa ni baina ya timu ya taifa ya Zanzibar Zanzibar Heroes kucheza dhidi ya timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars.
Katika mchezo wa pili wenyeji Uganda Uganda Crane watakuwa wakishuka dimbani dhidi ya Kilimanjaro Stars mchezo ambao utapigwa usiku baada ya mchezo wa nusu fainali ya kwanza.
Timu ya taifa ya Uganda Uganda Cranes itakuwa na kila sababu ya kutaka kutetea taji lake hii leo kutokana na ukweli kwamba itakuwa ikicheza ikiwa katika uwanja wa nyumbani mbali na kuwa itakuwa ikishangiliwa na mashabiki wake kibao ambao wanaingia bure uwanjani  Mandela kitongoji cha Namboole.
Timu hizi zimesha kutana mara tatu katika hatua kama hii ya nusu fainali baada ya kukutana 2010 na 2011. Uganda ilishinda mwaka jana kwa mabao 3-2 mwaka jana ilihali Kilimanjaro Stars ikishinda mwaka 2010 kwa njia ya penati 5-4.
Mpaka kufikia hatua hii ya nusu fainali, Uganda iliiondosha Ethiopia kwa mabao 2-0 katika robo fainali jumanne kule Namboole wakati ambapo Kilimanjaro ikiifungisha virago Rwanda kwa ushindi kama huo jumatatu kule Lugogo.
Kocha Kim Poulsen anatarajiwa kutokibadilisha sana kikosi chake ambapo mlinda mlango Juma Kaseja atakuwa kiongozi wa kikosi, matarajio ni kuwa ataendelea kuwatumia walinzi Amir Maftaha, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani na kitasa ni kama kawaida Shomari Kapombe.
Viungo ni Frank Dumayo, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar  washambuliaji watakuwa ni Mrisho Ngasa, Simon Msuva ambao watakuwa wakimsaidia mshambuliaji wa kati wa pekee John Boko.
Uganda Cranes inatarajiwa kumtumia mlinda mlango Hamza Muwonge huku kocha Bobby Williamson akitarajia kutumia ukuta wake ambao haujaruhusu bao mpaka sasa ukiongozwa na Denis Guma na Godfrey Walusimbi upande wa pembeni na sehemu ya kati ya ulinzi akitarajia kuwatumia Isaac Isinde na Henry Kalungi.
Viungo ni Hassan Wasswa, Geoffrey Kizito Baba na Moses Oloya.
Williamson bila shaka ataendele kuwatumia, Hamis Kiiza na Robert Ssentongo ambao katika michezo miwili ya hivi karibuni walionyesha kuchangamka zaidi.
Sambamba na hao kocha huyo anatarajia kumtumia Emmanuel Okwi ambaye amepewa kazi ya kuwanyonga Kilimanjaro kwa kuwa anawafahamu vema akisaidiwa na Brian Umony

No comments:

Post a Comment