Pages

Wednesday, December 19, 2012

LINA MHANDO AREJEA TENA TWFA



MGOMBEA Lina Kessy leo ameweza kutetea nafasi yake ya Uenyekiti katika uchaguzi  wa Chama cha Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA) unaliofanyika kwenye hoteli ya Midlands mjini Morogoro.

Akizungumza jijini Ofisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura alisema kuwa Lina amewashinda wenzake Isabela Kapera na Joan Minja katika uchaguzi huo kwa kukusanya kura 25 kati ya 50 zilizopigwa, huku Isabela akipata kura 13 na Joan 11.
Wambura alisema kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Rose Kissiwa aliweza kupita katika kinyanganyiro hicho kwa kujikusanyia kura 35  huku 13 zikisema hakuna na kura 2 zikiharibika.

Ofisa huyo alisema kuwa Amina Karuma ameshika nafasi ya Ukatibu mkuu na kumshinda mpinzani wake  Cecilia Mkafum baada ya kupata kura 35 huku mpinzani wake akipata kura 15.

Mwandishi mwaandamizi Zena Chande ambaye alikuwa mgombea pekee katika uchaguzi huo katika nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF aliweza kupata kura 24 huku kura 22 zikimkataa na 4 zimeharibika.

Huku nafasi ya mjumbe wa kamati ya Utendaji wa chama hicho ikienda kwa Triphonia Temba baada ya kumshinda mpinzani wake Sophia Charles baada ya kukusanya kura 39 huku Sophia akipata kura 30

1 comment:

  1. Hongera Amina. Mungu akupe nguvu, ujasiri na maarifa uweze kuikabili kazi iliyo mbele yako.

    ReplyDelete