Pages

Monday, December 17, 2012

HATIMAYE LULU ASOMEWA SHTAKA LA KUUA BILA KUKUSUDIA


KESI ya mauaji inayomkabili msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael (Lulu), dhidi ya aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba, imeendelea leo na Lulu amesomewa rasmi shtaka lakuua bila kukusudia

Lulu yuko rumande kwa miezi nane sasa kutokana na makosa ya mauaji na kukosa dhamana, anadaiwa kwamba Aprili 7 mwaka huu maeneo ya Vatican, Sinza, alimuua Steven Kanumba.

Kuchelewa kukamilika kwa upelelezi kulianza kuzua mjadala kwa watu mbalimbali wanaofika kusikiliza kesi hiyo, wakidai kwamba hawajui matukio gani nchini ambayo upelelezi wake unaweza kufanywa kwa haraka.

No comments:

Post a Comment