MUIGIZAJI Danniella Westbrook,amevunja ukimya akisema kuwa alibwia unga wakati akijifungua mwanawe wa kiume aitwaye Kai.
Nyota huyo wa zamani alitoa taarifa hiyo juzi katika kipindi cha mahojiano na watu mashuhuri kiitwacho Jeremy Kyle Show kinachorushwa na kituo kimoja cha televisheni cha nchini Uingereza.
Muathirika huyo wa zamani ambaye ameachana na matumizi ya dawa hizo takribani miaka 12 iliyopita, alimwambia mwandaji wa kipindi hicho, Jeremy kuwa alibwia unga huo muda mfupi kabla ya kujifungua katika choo cha chumba alichojifungulia :"Nilikula unga muda mfupi kabla ya kujifungua,"alisema nyota huyo wa zamani.
Alipohojiwa na Jeremy kama alikuwa akila unga kwa kipindi chote alichokuwa mjamzito mwanamama huyo alikiri akisema kuwa ni kweli na alikuwa akifanya hivyo kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment