BINGWA wa zamani duniani wa ngumi za kulipiwa katika uzani wa juu, David Haye ameamua kuingia tena darasani kujifunza sanaa ya maigizo ili aweze kuwa kama Arnold Schwarzenegger.
Bodia huyo alisema juzi kuwa tangu miaka mitano iliyopita alishatangaza kiu yake hiyo ya kutaka kuwa muigizaji mahili.
“Katika kipindi cha muda wa miaka mitano iliyopita mara zote nimekuwa nikisemakuwa nataka kuwa muigizaji mahili,ni lazima mara zote uwe na malengo ni mahali gani utakapokwenda,"alisema Haye.
Alisema kuwa japokuwa kipindi cha miaka mitano ni kirefu lakini ni lazima ufikiea malengo hayo.
Bondia huyo alisema kuwa ataanza fani hiyo kuanzia mwakani na mawazo yake yote yapo katika tasnia hiyo ili aweze kuwa muigizaji mahiri.
No comments:
Post a Comment