WINGA wa Crystal Palace
mwenye thamani ya pauni milioni 20, Wilfried Zaha (20) amejumuishwa kwenye
kikosi cha England, kitakacho cheza pambano la kirafiki dhidi ya Sweden,
Jumatano hii.
Wayne Rooney, Theo
Walcott, Jonjo Shelvey, Kyle Walker, Aaron Lennon, Jermain Defoe na Alex
Oxlade-Chamberlain watakosa mechi hiyo itakayochezwa Stockholm, Sweden kutokana
na majeruhi.
Kutokana na kukosekana
kwa wachezaji hao, Roy Hodgson ameamua kumuita kinda huyo mzaliwa wa Ivory
Coast kuziba baadhi ya nafasi zilizoachwa na mastaa hao.
Zaha amekuwa akitajwa
kama mmoja wa wachezaji wenye vipaji vikubwa sana anayeibukia kwenye soka la
England na amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu kadhaa kubwa za ligi kuu huku
Arsenal wakionekana kuongoza mbio za kumsajili.
No comments:
Post a Comment