Pages

Wednesday, November 14, 2012

TAIFA STARS YAWAPA RAHA WATANZANIA


Kwa Harambee stars huu ni mchezo wao wa pili kupoteza katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita ambapo mwezi Oktoba ilifungwa mabao 2-1 na Afrika Kusini mchezo uliofanyika jijini Nairobi.
Hii leo Harambee Stars ilikuwa ikiongozwa na mshambuliaji wake Denis Oliech akisaidiana na wakali kama Ayubu Timbe, Masika Jerry Santo na James Wakhungu Situma,  ambapo ilikuwa ikicheza mchezo wa kasi na kujiamini zaidi karibu sehemu kubwa ya mchezo lakini hata hivyo utulivu wa wachezaji wa Stars uliwasaidia katika kuharibu mipango ya Harambee Stars.
 Baada ya mchezo huo kocha wa Taifa Stars Kim Poulsen alikipongeza kikosi chake kwa kusema wamecheza mchezo mzuri licha ya mazoezi ya muda mfupi.
Amekiri Harambee Stars ni timu nzuri lakini nidhamu ya kimchezo ya vijana wake imesaidia kuweza kuwadhibiti wapinzani wao.
  Amesema kuelekea katika michuano ya Challenge atakuwa na muda wa kutosha wa kufanya maandalizi mazuri zaidi kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ambayo safari hii yatafanyika nchini Uganda.
Kwa upande wake kocha wa Harambee Henri Michel amesema kikosi chake kimecheza mchezo mbovu katika mchezo wa leo na kwamba kabla ya michuano ya Challenge atalazimika kufanya mabadiliko makubwa katika kuimarisha kikosi hicho. 
Taifa Stars baada ya mchezo wa jana itakuwa imebadili jina na sasa kuitwa Kilimanjaro Stars na itaendelea kuwepo mkoani Mwanza ikiendelea na maandalizi yao kabla ya kuelekea nchini Uganda tayari kwa michuano ya Kombe la Challenge ambapo Tanzania Bara itakuwa katika kundi moja pamoja na Burundi, Sudani Kaskazini pamoja na Somalia.
Wachezaji Nasoro Chollo na Aggrey Moris wanatarajiwa kuondoka katika kambi ya timu hiyo leo na kuelekea Zanzibar kujiunga wa wenzao katika kambi ya timu ya Taifa ya Zanzibar inayojiandaa kwa ajili ya michuano ya Challange.
  Kikosi cha Stars Kilichoanza dhidi ya Harambee Stars: Juma Kaseja, Kelvin Yondani, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomali Kapombe, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto na Thomas Ulimwengu.

 Wachezaji waliotokea benchi ni pamoja na Shabani Nditi, Simon Msuva, John Bocco, Amri Kiemba na Issa Rashidi.

No comments:

Post a Comment