Pages
▼
Thursday, November 29, 2012
TAIFA QUEENS YAPAA LEO KWENDA SINGAPORE KUSHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA YA MABARA
TIMU ya Taifa ya Netiboli ‘Taifa Queens’ imeondoka nchini leo saa tisa kuelekea nchini Singapore kwenye michezo ya kimataifa inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho kutwa na kumalizika Disemba 8 mwaka huu nchini humo.
Kikosi cha timu hiyo chenye wachezaji 12 pamoja na viongozi wawili kimeagwa leo na kukabidhiwa bendera na Naibu Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo Juliana Yasoda.
Akizungumza na jijini mara baada ya kuagwa, Katibu Mkuu wa Chama Cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Rose Mkisi alisema kuwa timu hiyo imeongozana na Mwenyekiti wa CHANETA na Daktari katika safari hiyo.
Mkisi alisema timu ikitua itaendelea na mazoezi baada ya mapumziko ya siku moja.
Kikosi hicho kinachoundwa na wachezaji kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kilipata maandalizi ya kutosha baada ya kukaa kambini mjini Morogoro kujiandaa na michuano hiyo.
Mkisi aliongeza kuwa kikosi hicho kinatarajiwa kufanya vizuri katika michuano zinazoshiriki timu kutoka kwenye shirikisho la Kimataifa la Netiboli (IFNA) kwa nchi itakayofanya vizuri ambapo Tanzania ipo nafasi ya tatu kwa Kanda ya Afrika.
No comments:
Post a Comment