Pages

Saturday, November 10, 2012

SIMBA NA AZAM ZAMALIZA MZUNGUKO WA KWANZA KWA KUFUNGWA

Beki wa Toto African Elly Hamad akimdhibiti Haruna Chanongo wa Simba kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa leo uwanja wa taifa

Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi akiwa amedhibitiwa na kiungo  wa Toto African  Peter Mutabuzi kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa leo uwanja wa Taifa
 


Kiungo wa Simba Amri Kiemba akimtoka beki wa Toto African kwenye mchezo uliochezwa taifa

Wachezaji wa Toto wakimpongeza mfungaji wa bao lao baada ya mchezo waliocheza leo kwenye uwanja wa taifa na Simba baada ya mchezo kumalizika.

TIMU ya Simba leo imemaliza mzunguko wa kwanza kwa kufungwa na Toto African bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Bao pekee la Toto lilifungwa na Mussa Said Kimbu dakika ya 73.

Kimbu alifunga bao hilo baada ya kupiga direct free kick baada ya kutokea faulo na kuwaacha  mabeki wa Simba na kipa wao, Wilbert Mweta wasijue cha kufanya.

Michezo mingine ya ligi iliyochezwa leo ni: Azam na Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Azam imefungwa 2-1.
Kwa matokeo haya, Yanga inazidi kukaa kileleni kwa pointi zake 26 na kesho itamaliza mechi yake ya mzunguko wa kwanza kwa kucheza Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Simba inaendelea kubaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 23 na Azam yenye pointi 24 ni ya pili.

Simba SC: Wilbet Mweta, Nassor Masoud ‘Chollo’, Paul Ngalema, Komanbil Keita, Shomari Kapombe, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngassa, Felix Sunzu na Emanuel Okwi. 

Toto African; Erick Ngwengwe, Ally Ahmad, Eric Murilo, Evarist Maganga, Peter Mutabuzi, Hamisi Msafiri, Emanuel Swita, Kheri Mohamed, Mohamed Jingo, Suleiman Kibuta na Mussa Said

No comments:

Post a Comment