TIMU ya Shein Rangers inayoshiriki ligi ya vijana waliochini ya miaka 17 ya mkoa wa Dar es Salaam jana iliifunga DAYSA bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa juzi mchana kwenye uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao wachezaji walionekana wanavipaji vya soka iliwachukua Shein Rangers dakika 7 na sekunde 12 kupata bao kupitia kwa Abdul Said.
Timu zote zilifanya mabadiliko ambapo Shein Ranger waliwatoa Hamza Mwalimu, Lukinga Abdul na Yassin Wito na wakaingia Athuman Mohamed, Hassan Idd na Edward Thomas.
DAYSA waliwatoa John Wiliam na Godfrey Andrea na waliingia Jimmy Michael na Steven Daniel.
Akizungumza baada ya mchezo kumalizika Katibu mkuu wa Chama cha Kuendelea vipaji (DAYOSA), Mwinyimad Tambaza alisema kuwa ligi inaendelea vizuri na timu zinaonyesha ushindani.
"Nashukuru ligi ya YOSO inaendelea vizuri na timu zinaonyesha ushindani wa kweli", alisema Tambaza.
No comments:
Post a Comment