Mshambuliaji wa Serengeti boys Husein Twaha akipambana na Abassi Juma kwenye mchezo wa kirafiki uliocghezwa uwanja wa taifa jana na Serengeti kushinda bao 2-1. |
TIMU ya Taifa ya Vijana waliochini ya miaka 17, "Serengeti boys" jana waliibuka kidedea baada ya kuifunga Falcon ya Zanzibar mabao 2-1 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa kusisimua kutokana na timu zote kutandaza kabumbu safi ulishuhudia timu zote kwenda mapumziko bila kufungana.
Kipindi cha pili kiianza kwa timu zote kufanya mabadiliko lakini Serengeti boys ndio waliweza kunufaika kwani dakika ya 74 walipata bao kupitia kwa Tumaini Baraka.
Baada ya kupata bao hilo Serengeti boys walizidisha mashambulizi na walionyesha wana kiu ya kutafuta mabao zaidi na dakika ya 82 mshambuliaji Farid Musa alifunga bao kwa shuti la mbali baada ya kumwona golikipa wa Falcon ametoka golini.
Katika kuhakikisha hawatoki uwanjani bila bao wachezaji wa Falcon walifanya shambulizi moja na nahodha wa Serengeti boys Miraji Adam akijifunga wakati akiokoa.
Kocha wa Falcon, Mohamed Mzee alisifu kikosi chake kwa mchezo ila alisema viungo walishindwa kukaa na mpira hali iliyofanya Serengeti boys kutumia nafasi hiyo kuwashambulia.
"Timu imejitahidi kucheza vizuri kwani tumecheza na timu yenye wachezari bora, ila viungo walishindwa kukaa na mpira na kusababisha tushambuliwe", alisema Mzee.
Jakob Michelsen alikipongeza kikosi chake kwa kucheza vizuri kwani wamecheza na timu nzuri
No comments:
Post a Comment