Monday, November 12, 2012
ARUSHA BINGWA SLAM SPRITE
TIMU ya kikapu ya mkoa wa Arusha jana iliibuka ubingwa wa Slam Sprite baada ya kuifunga Dodoma kwa vikapu 11 kwa 8.
Mashindano hayo ambayo yalianza kuchezwa mikoani yameweza kuibua vipaji vingi ambavyo vitakuwa tunu kwa taifa.
Awali akizungumza, Katibu wa Shirikisho wa Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Michael Maluwe, aliishukuru Kampuni ya Cocala kupitia kinywaji chake cha Sprite kwa kufanikisha mashindano.
Maluwe alisema kupitia kampuni hiyo wameweza kuona nyota ambao watalisaidia taifa kwenye mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi.
"Makampuni mengine yaige mfano kwa Copa Cocala ili kuinua michezo Tanzania", alisema.
Arusha iliibuka bingwa kwenye mchezo wa wachezaji watano na kupewa kombe, fulana na kofia huku Dodoma wao wakiondoka na Ipod kila mchezaji,fulana na kofia.
Kwenye mchezo wa wachezaji watatu kila timu Dodoma iliifunga Arusha vikapu 10 kwa 5 na kufanikiwa kutwaa ngao, fulana na kofia na Arusha kila mchezaji kuondoka na ipod, kofia na fulana.
Kwa upande wa street dancing mkoa wa Kilimanjaron walishinda na kupewa ngao.
Mikoa ambayo ilishiriki katika mashindano hayo ni Arusha, Dodoma, Kilimanjaro, Mwanza, Mbeya pamoja na Dar Es Salaam.
Mkoa wa Dar es salaam hakuweza kufurukuta kwani uliondolewa kwenye makundi kwa kufungwa na Kilimanjaro vikapu 15 kwa 11 na baadae kupotea kabisa baada ya kufungwa na Dodoma vikapu 28 kwa 12.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment