Pages

Monday, November 12, 2012

POLISI MARA YAZINDUKA, RHINO MWENDO MDUNDO, MAJIMAJI YABANWA NYUMBANI

TIMU ya Polisi Mara jana  ilizinduka usingizi na kuifunga wachovu wa kundi C Morani ya Manyara mabao 3-1 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Karume, mkoani Mara.

Mabao ya Polisi yalifungwa na Daniel Mayeye dakika ya 13, Yohana Mirobo dakika ya 29 na Hamis Hamza dakika ya 68 na bao la Morani lilifungwa na Amiry  Msuwa dakika ya 76.

Michezo mingine iliyochezwa kwenye kundi C ni kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, ambapo Polisi Tabora walitoka sare ya 0-0 na Mwadui ya Shinyanga

Uwanja wa Lake Tanganika Kigoma Kanembwa ilishindwa kuutumia uwanja wa nyumbani baada ya kutoka sare ya 0-0 na Pamba ya Mwanza.

Kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma, maafande wa Polisi Dodoma walishindwa kuhimili gwaride la maafande wa jeshi la wananchi kwa kukubali kipigo cha mabao 2-0 nyumbani.

Kundi A uwanja wa Majimaji mjini Songea, Majimaji na Mlale zote za Ruvuma zilitoka sare ya bao 1-1

Bao la Majimaji lilifungwa na Edward Songo dakika ya 70 kwa kichwa na la Mlale lilifungwa na Chale Haule kwa penalti dakika ya 85.

No comments:

Post a Comment