LIONEL Messi ameweka
rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote ndani ya mwaka mmoja baada ya kufunga
kwenye pambano ambalo Barcelona walishinda dhidi ya Real Mallorca na kutimiza
mabao 76 mwaka 2012.
Messi, (25), ameifungia
Barcelona mabao 64 na Argentina mabao 12 mwaka huu pekee na kufanikiwa kuivuka
rekodi ya mabao 75 kwa mwaka iliyokuwa ikishikiliwa na gwiji wa Brazil, Pele.
Mpaka sasa Muagentina
huyo ana zaidi ya mabao 300 aliyofunga katika maisha yake ya sasa ya soka na kwa
sasa anaongoza orodha ya wafungaji ya La Liga msimu huu akiwa amefunga mabao 15
katika mechi 11.
Messi aliifungia Barcelona
bao la pili na la nne juzi na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao
4-2 dhidi ya timu ngumu ya Mallorca.
Kocha wa Barcelona, Tito
Vilanova amesifia uwezo mkubwa wa kufunga mbao wa Messi kwa kusema kwamba siyo
mabao yote anayofunga mchawi huyo wa Soka ni rahisi.
Pamoja na kufunga mabao
manne, Vilanova alifedheheshwa na jinsi timu yake ilivyofanya makosa mengi ya
wazi ambayo yaliwaponza na kuruhusu mabao mawili.
No comments:
Post a Comment