Pages

Monday, November 5, 2012

MATOKEO YA LIGI DARAJA LA KWANZA JUZI


TIMU ya Rhino ya Tabora juzi iliutumia vema uwanja wake wa nyumbani kwa kuibamiza Kanembwa Fc ya Kigoma mabao 3-1 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Rhino ilijipatia mabao yake kupitia kwa Bakari Mahadhi dakika ya 26, Shija Kanju dakika ya 29 na Abdallah Simba dakika ya 64 na Kanembwa wao walipata bao ku[pitia kwa Ally Bilal dakika ya 62.

Michezo mingine iliyochezwa kwenye kundi C ni kati ya Polisi Tabora na Polisi Mara kwenye uwanja wa Karume mkoani Mara mbao walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Goli la Polisi Mara lilifungwa na Daniel Manyenye na Polisi Tabora lilifungwa na Ernest Mkali

Uwanja wa Kambarage Shinyanga Mwandui iliifunga Pamba FC ya Mwanza 2-0

Huko Kiteto mkoani Manyara Moran na Polisi Dodoma walitoka sare ya 1-1.

Michezo ya kundi A, Uwanja wa Samora mkoani Iringa Polisi Iringa ilifunga Majimaji ya Ruvuma mabao 4-3.

Polisi Iringa walijipatia mabo yake kupitia kwa Ramadhan Kidunda aliyefunga mawili dakika ya 11 ya 75, Sayuni Mtunjulwa dakika ya 40 na Nissa Mwandani dk 64.

Majimaji mabao yao yalifungwa na Peter Mapunda aliyepachika mawili dakika ya 36 na 51  na Sixmund Mwasekiga  dakika 71

Huko Makambako kwenye uwanja wa Wambi Burkina Faso ya Morogoro waliifunga kurugenzi ya 1-0.

Goli la Burkina Faso lilifungwa na Jamwaka Buya dakika ya 78.

Mjini Songea kwenye uwanja wa Majimaji Mlale na Mkamba walitoka 0-0

Kwenye uwanja wa Mandela mkoani Rukwa wenyeji Small Kids walifungwa na Mbeya City mabao 3-0.

Katika hali ambayo siyo ya kawaida mashabiki waliokuwepo uwanjani hapo walikuwa wakiizomea sana Small Kids kwa madai siyo timu yao hivyo kufungwa kwao kulikuwa ni furaha kwa wenyeji.

No comments:

Post a Comment