Kikosi cha Yanga |
Ligi kuu ya Tanzania Bara imeendelea hii leo katika uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba ambapo timu ya Yanga imeambulia kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa wakata miwa wa Kagera Sugar.
Bao
la Kagera Sugar limepatikana kipindi cha pili cha mchezo dakika ya 70,
Bao hilo limefungwa na mchezaji mahiri mzaliwa wa Kimbugu Muleba Temmy
Alfonce.
Huu unakuwa mwanzo mbaya kwa kocha mpya wa Yanga Erneus Brandts
ambaye ni raia wa Holland ambapo mechi ya kwanza aliambulia suluhu
dhidi ya Simba na leo kupata kichapo cha goli kwa moja kwa bila dhidi Kagera sugar .
No comments:
Post a Comment