Pages

Friday, October 19, 2012

UMOJA WA MATAIFA KUKIPIGA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KESHO LEADERS






TIMU ya soka ya ofisi ya Umoja wa Mataifa kesho asubuhi watakuwa na mchezo wa kirafiki na timu ya Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimatifa kwenye uwanja wa Leaders Club Kinondoni.

Mchezo huo ni sehemu ya shamrashara za kuadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa ambayo husheherekewa Octoba 24 kila mwaka.

Akizungumza na LENZI YA MICHEZO, Katibu wa timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Japhet Chaula alisema kuwa Ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyopo hapa nchini wameandaa mchezo huo katika kuadhimisha siku yao ikiwa na lengo la kufahamiana na kubadilishana mawazo kwani baada ya kucheza watakuwa na tafrija fupi kwenye viwanja vya Leaders.

"Umoja wa Mataifa wameandaa mchezo huu ili kujenga mahusiano ikiwa ni pamoja na kufahamiana na kubadilishana mawazo katika kazi na mambo mengine", alisema Chaula.

Shamrashamra za siku ya Umoja wa Mataifa zimeanza Octoba 19 mwaka huu kwa kufanya shughuli za kijamii na zitafika tamati 0ctoba 24 mwaka huu kwa kupandisha bendera ya umoja wa Mataifa kwenye ofisi za serikali na taasisi zake.

No comments:

Post a Comment