Pages

Friday, October 19, 2012

TWFA ORODHA YA WAPIGA KURA


Joan Minja mmoja wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa TWFA

KAMATI ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) imewataka wanachama wa TWFA ambao ni mikoa ya Tanzania Bara kuwasilisha orodha ya wajumbe wao wa mkutano wa uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa kamati hiyo Ombeni Zavala Wajumbe ni Mwenyekiti, Katibu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TWFA kutoka vyama vya mikoa ambayo tayari imefanya uchaguzi.

Pia alisema Mikoa ambayo imeshafanya uchaguzi mpaka sasa ni Iringa, Kigoma, Mwanza, Pwani na Tanga na alihimiza mikoa ambayo haijafanya uchaguzi kufanya uchaguzi kwani mwisho wa kutuma majina ya wajumbe ni Oktoba 25 mwaka huu.

Zavala alisema Mkoa ambao utakuwa haujafanya uchaguzi utakuwa umejinyimwa haki ya kushiriki uchaguzi wa TWFA utakaofanyika Novemba 4 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment