Pages

Wednesday, October 10, 2012

SIMBA YAIBANJUA AZAM

Wachezaji wa Simba wakiwa kwenye benchi uwanja wa Taifa

TIMU ya Simba jana asubuhi iliifunga Azam FC mabao 3-2 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Azam Complex uliopo Mbande Chamazi.

Simba ambao iliwatumia baadhi ya wachezaji wa timu "B" na wale waliopo kikosi cha kwanza lakini wanaanzia benchi, waliutumia mchezo huo kama maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Octoba 13, mwaka huu, uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Simba ambao walionekana kucheza vizuri ilijipatia bao lake la kwanza kupitia kwa mshambuliaji chipukizi Ramadhan Singano, "Messi", Uhuru Suleman na Daniel Akuffo.

Mabao yote ya Azam yalifungwa na mshambuliaji wao kinda Hamis Mcha, moja lilitokana na pasi yake kumbabatiza beki wa Simba na kutinga wavuni.

Kocha msaidizi wa Azam Kally Ongala alisema mchezo huo wanautumia kama maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Polisi Morogoro utakaochezwa uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Pia alizitaka timu zingine hasa Yanga wakubali kucheza nao pindi watakapowaomba kwani inasaidia kuipa uzoefu.

Naye Ofisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alisema, ushindi dhidi ya Azam ni ishara tosha kuwa Coastal Union siku ya Jumatano watapata kipigo japo wapo nyumbani kwao.

No comments:

Post a Comment