Timu ya Simba B imeifunga Moro United ambayo ipo daraja la kwanza mabao 3-0 katika mchezo wa uliochezwa mchana kabla ya mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Simba na Kagera Sugar, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanza.
Mabao ya Simba B inayofundishwa na Suleiman Matola, akisaidiwa na Amri Said ‘Stam’ yalipatikana kipindi cha pili na wafungaji ni Ramadhan Salum dakika ya 65 na 70 na Miraj Athumani dakika ya 85.
Moro United inajiandaa na Ligi Daraja la Kwanza, inayotarajiwa kuanza Oktoba 24, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment