Pages

Monday, October 22, 2012

PAMBANO LA YANGA, RUVU SHOOTING LAINGIZA MIL 47/-


Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Ruvu Shooting lililochezwa Oktoba 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa wenyeji Yanga kushinda mabao 3-2 limeingiza sh. 47,615,000.
 
Watazamaji 8,233 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000, na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 8,420,578.47 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 7,263,305.08.
 
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 120,000, kamishna wa mechi sh. 203,000, waamuzi sh. 381,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
 
Umeme sh. 300,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 3,500,000 wakati tiketi ni sh. 2,959,100. Gharama za mchezo sh. 2,806,859.49, uwanja sh. 2,806,859.49, Kamati ya Ligi sh. 2,806,859.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,684,115.69 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,122,743.80.
 

No comments:

Post a Comment