Pages

Saturday, September 22, 2012

YANGA YANG'AA NA MTIBWA YANG'ANG'ANIWA CHAMAZI

Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la Kwanza alilofunga Nadir Haroub kwenye mchezo wao na JKT Ruvu taifa leo

Beki wa JKT Ruvu Stanley Nkomola akimtoka mshambuliaji wa Yanga Didier Kavumbagu wakati wa mchezo wao uliochezwa leo Taifa na Yanga kushinda bao 4-1


Hamis Kiiza akipambana na beki wa JKT Ruvu Sostenes Manyasi kwenye mchezo leo

TIMU ya Yanga ya Dar es salaam leo imezinduka usingizi na kuipatia kichapo JKT Ruvu bao 4-1 kwenye uwanja wa taifa mbele ya Yusuf Manji.

Yanga ambayo ilicheza kwa kujiamini sana na kushambulia muda wote ilijipatia mabao yake kupitia kwa Nadir Haroub Canavaro, Didier Kavumbagu ambaye alifunga mawili na Mshambuliaji Kinda Simon Msuva alihitimisha idadi ya mabao.

Michezo mingine iliyochezwa ni Azam 1 vs Mtibwa 0 ulichezwa Chamazi
JKT Oljoro 1 vs Polisi Moro ulichezwa Sheikh Aman Karume Arusha
Toto African 1 vs Coastal Union ulichezwa Mkwakwani Tanga.

Kesho kutakuwepo na michezo ya
Simba vs Ruvu Shooting utakaochezwa Uwanja wa Taifa
Mgambo JKT vs Kagera Sugar uwanja wa Mkwakwani Tanga
African Lyon vs Tanzzania Prison uwanja wa Chamazi

No comments:

Post a Comment