Pages

Friday, September 21, 2012

THOMAS ULIMWENGU ANG'ARISHA TP MAZEMBE

Mshambuliaji Thomas Ulimwengu
MSHAMBULIAJI chipukizi wa Tanzania Thomas Ulimwengu anayechezea timu ya TP Mazembe ya Demokrasia ya Congo (DRC) juzi aliifanya timu yake ishinde 2-1 kwenye mchezo wa ligi.

TP Mazembe iliyokuwa inakipiga na SC Makiso ya nchini humo walishinda mchezo huo baada ya mshambuliaji Tresor Mputu kufunga bao la kwanza na Thomas Ulimwengu kuitimisha kwa kufunga bao la pili na la ushindi.

Thomas Ulimwengu ambaye yupo kwenye timu ya Taifa (Taifa stars) ameonyesha kuwa alistahili kuingizwa kwenye kikosi kikubwa cha TP Mazembe kwani amekuwa akifanya vizuri kila anapocheza.

Mchezo huo ulichezwa kwenye uwanja Stade Lumumba uliopo Kisangani, ambapo SC. Makiso wanashika nafasi ya 14 wakiwa na pointi 9.

TP Mazembe ambayo ipo nafasi ya tatu na ina pointi 40 kwenye msimamo wa ligi ya DRC nyuma ya Motema ya Pembe yenye pointi 42 na kinara wa ligi ni V.Club yenye pointi 47.

No comments:

Post a Comment