Pages

Friday, August 24, 2012

Add caption

UONGOZI wa chama cha soka manispaa wa Iringa (IMFA) unatarajia kuendesha mashindano ya Jesca cup yatakayofunguliwa kesho kwenye uwanja wa Samora.

Akizungumza na HABARI ZA MICHEZO kwa njia ya simu katibu wa IMFA Rashid Shungu alisema mashindano hayo yatashirikisha timu 30 toka manispaa na yatachezwa katika kanda tano.

Pia alisema mashindano hayo ambayo yanafunguliwa na mkuu wa wilaya ya Iringa yana lengo la kuendeleza soka na kufanya timu za daraja la nne zijiandae vizuri.

Katika kila kanda zitatoka timu mbili ambazo zitaunda timu kumi bora na kila timu ya kwanza kwenye kanda itapewa seti moja ya jezi na mipira miwili na ya pili itapewa mipira miwili.

Alisema mfadhili wa Jesca cup aliamua kutoa vifaa kwa kila timu zilizotinga kumi bora ili zijiandae vizuri kwani hatua hii itakuwa ni ya mtoano.

"Kila kanda itatoa timu mbili ambazo zitashiriki kucheza kumi bora ambapo itachezwa kwa mtoano" alisema Shungu.

Shungu alisema mshindi wa kwanza atapata kombe, shilingi 300,000 na mipira miwili, mshindi wa pili atapata ngao, shilingi 300,000 na mpira mmoja na mshindi wa tatu atapata sh 300,000 tu.

Timu yenye nidhamu itazawadiwa shilingi 50,000 na mfungaji bora atapewa shilingi 16,000 na waamuzi watapewa sh 180,000.
***************************************************
TIMU ya Ashanti ya Ilala juzi iliifunga TAYSA ya Temeke bao 2-0 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Rovers Msimbazi Centre Ilala.

Ashanti ambayo inajiandaa kucheza ligi daraja la kwanza ilijipatia mabao yake kupitia kwa Abdul Mahmudu.

Naye Mratibu wa TAYSA academy Omar Shariff alisema ameridhika na kiwango kilichoonyeshwa na timu yake kwani uwanja una mchanga na wachezaji wake U-20.

"Timu yangu japo imefungwa na imecheza vizuri ila tatizo ni uwanja una mchanga" alisems Omar.

Pia alisema kuwa kituo chake kina timu za U-10, U-12, U-14, U-17 na U-20 na kinahudumia watoto yatima.

Naye kocha wa Ashanti Mubaraka alisema kuwa timu yake imecheza vizuri kwani hakutegemea kama ingeweza kucheza vizuri kwani walikuwa kwenye mazoezi magumu.

"Wachezaji wamecheza vizuri kwani wametoka kwenye mazoezi magumu na nilitegemea kuwa wafanye mazoezi ya kuweka mwili sawa", alisema Mubaraka.
***************************************************

Mabondia  wa Ilala wakimsikiliza kocha Habibu Kinyogoli



UONGOZI wa chama cha ngumi wilaya ya Ilala unawaomba wadau na watu wote wanaopenda michezo kusaidia kambi yao inayojiandaa na mashindano ya taifa yanayotarajiwa kuanza septemba 17 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Akizungumza na habari za michezo  ilipotembelea kambi hiyo ambayo ipo CCM Amana Rajabu Mhimila maarufu kama 'Super D' ambaye ni kocha mkuu alisema kambi yao ipi katika hali mbaya kwani mabondia hawana maji, nauli na mahitaji mengine muhimu.

"Mabondia wanatakiwa wapate maji wakati wakiwa mazoezini na nauli ya kuja na kurudi kwani pesa ya kupanga hoteli hatuna na matumizi mengine hivyo tunaomba wafadhili wajitokeze kutusaidia ili tuweze kuandaa timu vizuri", alisema super D

Pia alisema kwa yeyote ambaye ataguswa afike kwenye jengo la CCM Amana pia wadau wanaombwa wafike kuangalia mazoezi ili waweze kutoa ushauri kwa mabondia.

Super D alisema wanatarajia kupeleka mabondia wa uzito wa kg 51, kg 54, kg 66 na kg 72 kwenye mashindano hayo ambayo yatashirikisha mikoa yoye ya Tanzania.

Nao mabondia walisema wapo tayari kwani makocha wao wanawafunza vizuri na Ilala inasifika kutoa mabondia wakali ila nao kilio chao kilikuwa ni wafadhili ili wacheze mapambano mengi kwani ndipo watapata uzoefu.
****************************************************************************

No comments:

Post a Comment