Kipa David De Gea
Manchester United wamekubali kumuuza David De Gea na kabla ya kumruhusu kwenda Real Madrid, wanajipanga kumsajili golikipa wa Atletico Madrid, raia wa Slovenia, Jan Oblak.
Gazeti la AS linadai Oblak ndiye mrithi wa David De Gea na Man United wanataka kukamlisha usajili huo na wameshaanza mawasiliano naye.
Oblak alitua Atletico Madrid msimu uliopita akitokea Benfica na alirithi mikoba ya Thibaut Courtois, ambaye aliondoka kwenda Chelsea.
No comments:
Post a Comment