Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, December 10, 2014

ARSENAL YAIFUNGA GALATASARAY 4-1 UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Aaron Ramsey Akipongezwa baada ya kufunga bao na wachezaji wenzake usiku huu kwenye mchezo wa Klabu Bingwa Ulanya hatua ya mwisho ya Makundi.Arsenal wameanza vyema leo kwenye Mchezo wao wa mwisho wa makundi huku wakiwa wamefudhu kuendelea katika hatua nyingine, Lukas Podolski alianza kuipa bao dakika ya mapema dakika ya 3. Aaron Ramsey aliongeza bao la pili dakika ya 11 na Aaron Ramsey kuifungia bao la tatu dakika ya 29 na Arsenal kwenda mapumziko wakiwa mbele ya bao 3-0 dhidi ya Galatasaray ambao wanapointi moja kwenye kundi lao D na wakiwa wa mwisho.
Hector Bellerin wa Arsenal akichuana na Hamit Altintop wa Galatasaray.
Bao la pekee la Gala lilifungwa dakika za mwishoni dakika ya 88 na Wesley Sneijder na Arsenal nao walifunga tena bao la mwisho dakika za majeruhi za nyongeza bao lao la 4 kupitia kwa Lukas Podolski tena na mtanange kumalizika kwa 1-4.Aaron Ramsey akimfunga kipa wa Gala Sinan Bolat bao la pili kwa  Arsenal
Mchezaji wa Galatasaray Umut Bulut  akichuana na kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny langoni mwake.

No comments:

Post a Comment