






Van Persie akiwekwa kati!

Robin van Persie aliifungia Manchester United Bao katika Dakika ya mwisho ya Dakika 4 za Majeruhi na kuipa Sare ya Bao 1-1 na Vinara wa Ligi Kuu England Chelsea.
Chelsea walitangulia kupata Bao kupitia Didier Drogba ambae alifunga kwenye Dakika ya 53 kwa Kichwa baada ya Kona ya Cesc Fabregas.

Ingawa Man United walimiliki zaidi Mpira na kulenga Mashuti mengi zaidi ya Chelsea lakini ule udhaifu wao wa Difensi, hasa kulinda Mipira ‘iliyokufa’ kumewagharimu kwa mara nyingine tena.

Huku Bango likiashiria zipo Dakika 4 za Nyongeza baada ya Dakika 90 kukamilika, Chelsea walibaki Mtu 10 katika Dakika ya 93 baada ya Branislav Ivanovic kulambwa Kadi ya Njano ya Pili kwa kumsukuma Angel Di Maria na kupewa Kadi Nyekundu.

Frikiki iliyofuatia ilipigwa na Angel Di Maria na kukikuta Kichwa cha Marouane Fellaini lakini Kipa Thibaut Courtois akaokoa na kumtemea Robin van Persie ambae alipachika Mpira wavuni na kuamsha shangwe kubwa Ndani ya Old Trafford.
Hata hivyo, Sare hii imewapaisha Chelsea kileleni wakiwa Pointi 4 mbele ya Timu ya Pili Southampton na Pointi 6 mbele ya Timu ya 3 Mabingwa Man City.

Man United wao wamebakia Nafasi ya 8 wakiwa Pointi 10 nyuma ya Chelsea.
Mechi inayofuata kwa Manchester United ni ule mtanange wa Dabi ya Manchester watakapotua Etihad kupambana na Mahasimu wao wakubwa Manchester City Jumapili Novemba 2.





De Gea, Rafael, Smalling, Rojo, Shaw, Blind, Fellaini, Januzaj, Di Maria, Mata, van Persie.
Chelsea XI
Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Felipe Luis, Fabregas, Matic, Willian, Oscar, Hazard, Drogba
Chelsea kuendelea kutema cheche tena leo?
Diego Costa wenda akacheza kipindi cha pili!
Radamel Falcao aliumia wenda hasicheze mtanange huu

No comments:
Post a Comment