Mbuyu Twite akitia dole gumba mbele ya Abdalah Bin Kleb |
Katibu
mkuu wa klabu ya FC Lupopo ya nchini Congo yuko nchini Tanzania kwa
lengo la kufuatilia malipo ya pesa za mkopo za mlinzi Mbuyu Twitte
ambaye ameongeza mkataba wa mwaka mmoja na klabu yake ya Yanga kufuatia
mkataba wake wa awali wa misimu miwili kumalizika.
Akiongea
na Rockersports katika mahojiano maalum, katibu mkuu wa FC Lupopo
aliyejitambulisha kwa jina la Constantine Kabika amesema klabu yake ya
Lupopo iliingia makubalino na Yanga ya kumsajili Mbuyu kwa mkopo wa
miaka miwili na kwamba kipindi hicho cha makubaliano ya mkopo tayari
kimemalizika.
Kabika
amesema FC lupopo imekuwa katika mawasilino na Abdalah Bin Kleb na
Seif Abdalah (maarufu Seif Magari) ambao hapo kabla wakiwa katika kamati
ya usajili ya Yanga ndio waliomsajili mchezaji huyo akitokea katika
klabu ya APR ya Rwanda lakini amekuwa akizungushwa juu ya suala hilo na
kwamba sasa FC Lupopo imeanza kuchukua hatua nyingine za kuishitaki
klabu hiyo shirikisho la soka nchini TFF na shirikisho la soka duniani
FIFA.
Mbuyu Twite pamoja na Haruna Niyonzima enzi hizo wakiichezea APR ya Rwanda kabla ya kujiunga na Yanga |
Amesema
ameshangazwa na viongozi hao kutaka kumpa yeye kama katibu kiasi cha
dola elfu tano ambazo yeye binafsi hakujua ni za nini kwakuwa makubalino
ni baina ya vilabu viwili ambavyo vilikubaliana malipo ya mchezaji huyo
kuwa dola elfu ishirini na mkataba baina ya vilabu hivyo upo TFF na
kwamba aliyekuwa mkurugenzi wa mashindano wa TFF Saad Kawemba
alishuhudia makubaliano hayo.
Katibu
huyo wa Lupopo fc, Kabisa amesema kinachomshangaza zaidi ni kuwa hata
baada ya mkataba huo kumalizika, bado Yanga imeendelea kumsajili mlinzi
huyo bila ya mawasiliano yoyote na Lupopo fc ambao kimsingi ni mchezaji
wao halali na kwamba walikubaliana wawasiliane baada ya mkataba huo
kumalizika endapo Yanga ingependa kuendelea kuwa naye, jambo ambalo
Yanga imeshindwa kutekeleza ilhali Mbuyu si mchezaji wa Yanga tena.
Amesema
amekuwa akifanya mawasiliano na mlinzi huyo ambaye kwasasa amekuwa
haonyeshi ushirikiano na yeye, huku habari za chini ya kapeti alizonazo
ni kuwa tayari Yanga imempatia kiasi cha dola elfu moja na mia tano za
kwake kama mchezaji na kumsainisha mkataba wa mwaka mmoja, huku wao
Lupopo fc wakiendelea kusumbuliwa na uongozi wa Yanga kupitia kwa
wajumbe wa zamani wa kamati ya Usajili Bin Kleb na Seif Magari.
Kabika
amefunguka zaidi kwa kusema FC Lupopo ina mkataba wa miaka minne na
Mbuyu Twite ambao utamalizika baada ya msimu huu na kwamba APR ya Rwanda
ilimuuza kimakosa mlinzi huyo kwa Yanga kwani wakati wanamuuza alikuwa
ndio kwanza ana mwaka mmoja ndani ya mkataba wake na FC Lupopo.
Ameitaka
Yanga kuilipa FC Lupopo pesa zao za mkataba wa mwaka mmoja wa mkopo
mwingine ili kuachana na malumbano baina yao huku wakiwa tayari
wamejipanga kuelekea mbali zaidi kunako shirikisho la soka dunia fifa na
lile la Afrika caf endapo hilo litashindikana.
No comments:
Post a Comment