TIMU ya Azam FC na Mbeya
City zimeendelea kuifukuzia Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania
Bara, baada ya zote kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Azam iliifunga Mtibwa Sugar
uwanja wa Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, huku Mbeya City ikiichapa
Kagare Sugar mjini Bukoba.
Ushindi huo umezifanya Azam
na Mbeya City zote kufikisha pointi 30, moja nyuma ya Yanga yenye pointi 31
baada ya kushuka dimbani mara 14.
Katika mchezo wa Azam na
Mtibwa, timu zote zilianza kwa kushambuliana kwa zamu, huku Azam ikionekana
kulisakama lango la Mtibwa kwa kasi zaidi, lakini uimara wa mabeki wake
waliweza kukoa hatari kadhaa.
Pasi iliyopigwa na Joseph
Kimwaga iliweza kumpata vizuri, Tchetche aliyefunga bao hilo pekee baada ya
kuweza kuwachomoka mabeki wa Mtibwa na kufumua shuti lililojaa moja kwa moja
wavuni.
Kikosi cha Azam kilikuwa;
Mwadini Ali, Malika Ndeule, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre
Balou, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Brian Umony/Ismael Kone
dk13/Khamis Mcha dk71, Kipre Tchetche na Joseph Kimwaga/Seif Karihe dk69.
Mtibwa Sugar; Hussein
Sharrif, Hassan Ramadhani, Said Mkopi, Salim Mbonde, Salvatory Ntebe, Shaaban
Nditi, Shaaban Kisiga, Masoud Ally/Abdallah Juma dk62, Juma Luizio/Mussa Mgosi
dk84, Jamal Mnyate na Vincent Barnabas/Mohamed Salum dk75.
Katika mchezo mwingine,
Coastal Union ilitoka sare ya kufungana bao 1-1, JKT Oljoro mchezo uliopigwa
uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
No comments:
Post a Comment