Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) imekutana Desemba 28, 2013 kujadili mambo
mbalimbali yaliyofikishwa mbele yake ikiwemo usajili wa dirisha dogo
ambapo klabu zenye matatizo zimepewa hadi Januari 10 mwakani
kurekebisha.
Baadhi
ya klabu ikiwemo Simba zimezidisha idadi ya wachezaji, hivyo zimepewa
hadi muda huo kupunguza ambapo zikishindwa kazi hiyo itafanywa na Kamati
yenyewe.
Simba ina nafasi tano za kujaza kwenye dirisha dogo lakini imewasilisha majina ya wachezaji sita.
Pia
klabu nyingine zimetakiwa ama kuvunja mikataba ya wachezaji au
kuendelea kuwa nao, na si kuendelea kuwalipa mishahara wakati
imeshawaondoa katika orodha yao.
No comments:
Post a Comment