Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, May 29, 2013

SSENKOOMI: OKWI AMENIFANYA NIJE SIMBA

BEKI Mganda, aliyesajili Simba, Samuel Ssenkoomi, amesema mafanikio ya fowadi wa Uganda, Emmanuel Okwi, ndicho kitu kilichomshawishi kukubali kumwaga wino kucheza soka kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Beki huyo wa kati, Ssenkoomi, alisema jana kwamba yeye hana ufahamu mzuri kuhusu soka la Tanzania na klabu ya Simba, lakini kutokana na kuwatazama Okwi na Mganda mwingine, kipa Abel Dhaira, ambao wanaichezea timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi, jijini Dar es Salaam, kumemfanya akubali kusaini kuichezea Simba msimu ujao.

Katika mahojiano hayo maalumu, beki huyo wa kikosi cha URA, alisema anakuja Simba kufanya kazi moja tu, kuonyesha ubora wake huku akiomba ushirikiano kutoka kwa wachezaji wenzake katika timu hiyo ili waweze kufanya kazi nzuri.
“Sina ufahamu mzuri juu ya Ligi Kuu ya Tanzania, lakini naamini kutakuwa na ushindani mkubwa kwa sababu nimeweza kuliona hilo kupitia wachezaji wengine kutoka Uganda, kama Emmanuel Okwi na Abel Dhaira, ambaye yeye alijiunga hapo mwaka jana," alisema.

Simba imemsajili beki huyo ili kumaliza tatizo la ulinzi kwenye kikosi chake, ambapo katika msimu wa Ligi Kuu Bara uliomalizika hivi karibuni, timu hiyo ilionekana kuwa na udhaifu mkubwa katika nafasi hiyo kiasi ambacho kimewagharimu na kumaliza msimu wakiwa katika nafasi ya tatu.

Ssenkoomi alisema kila kitu kimekamilika katika usajili wake na kwamba anachosubiri ni kutua hapa nchini ambapo atapata fursa ya kukutana na Mganda mwenzake, Dhaira katika kikosi hicho cha Msimbazi.
Fowadi aliyekuwa chachu kubwa ya beki huyo kusajili Simba, Okwi, kwa sasa anaichezea Etoile du Sahel ya Tunisia, timu aliyojiunga nayo mwaka jana.

Lakini, kubwa analosisitiza beki huyo ni ushirikiano kutoka kwa wenzake, kwa sababu anafahamu wazi mafanikio hayawezi kupatikana kwa kupitia mchezaji mmoja pekee.

No comments:

Post a Comment