Masanja Mkandamizaji apania Tamasha la UZINDUZI WA ALBUM ZA KAPOTIVE STAR SINGERS - BUKOBA.
Na Faustine Ruta, Bukoba
MCHEKESHAJI maarufu na mwimbaji wa muziki wa Injili nchini, Emmanuel Mgaya, Masanja Mkandamizaji, amesema kuwa amejipanga imara kuhakikisha kuwa anafanya vitu vya aina yake katika onyesho la Uzinduzi wa Albam mbili(2) za KAPOTIVE STAR SINGERS - BUKOBA, linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam , Katika Ukumbi wa UBUNGO PLAZA na kushirikisha pia wasanii wakali mbalimbali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,Masanja alisema kuwa amejiandaa vyema kutangaza neno la
“Nipo sawa kiafya na naamini Mungu atanibariki kila zuri kwa ajili ya kuimba pamoja kwenye tamasha hilo la KAPOTIVE STAR SINGERS - BUKOBA nikiwa na waimbaji wengine wenye makali ya aina yake kama Upendo Nkone na wengine wengi.
“Itakuwa ni siku nzuri siku ya Jumapili ya tarehe 5/5/2013 katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini, hivyo naamini watu watakuja kwa wingi kulishuhudia neno likipenya masikioni mwao,” alisema Masanja Mkandamizaji.
Mbali na Masanja, wengine watakaofanya onyesho hilo ni pamoja na KAKAU Band - Bukoba, Kwaya ya AIC-Chang'ombe, Kwaya ya Mt. Kizito Makuburi,Upendo Nkone
Kwaya ya AIC-Chang'ombe kutoka kushoto Mrs Gewe,Mr.Frank,mrs Lydia Kashimba na mrs Bahati MeshackKwaya ya Kapotive Star Singers - Bukoba
No comments:
Post a Comment