YAONEKANA hakuna
dawa mjarabu itakayokifanya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA)
kitawalike.
Kwa miaka mingi sasa, jitihada za serikali kuona soka
la Zanzibar linapiga hatua na kutambulika kimataifa, zimekuwa zikirudishwa nyuma
kutokana na migogoro isiyokwisha ndani ya ZFA.
Awali, kelele
za wadau zilikuwa zikielekezwa kwa viongozi wa chama hicho, wakidaiwa kuwa
hawana dhamira ya dhati kuiletea Zanzibar maendeleo katika mchezo wa mpira wa
miguu.
Kelele hizo zilimfanya Ali Ferej Tamim aliyekuwa Rais
wa chama hicho kwa zaidi ya miongo miwili, aamue kukaa pembeni na kuruhusu
kufanyika uchaguzi mdogo ili kupata Rais mwengine, ambaye alitarajiwa kushusha
presha za wadau waliokuwa wakililia mabadiliko.
Hatimaye,
Juni 30, mwaka jana, ZFA ikaitisha uchaguzi mdogo uliomuweka madarakani Amani
Ibrahim Makungu kuwa Rais kwa kipindi kilichobakia kabla ya uchaguzi mkuu wa
Disemba 2014.
Yalikuwa matumaini ya wengi, hata viongozi wakuu wa
Serikali ya Zanzibar ambao hawakusita kuelezea kuchoshwa kwao na migogoro ya ZFA
kila walipopata nafasi, kwamba sasa mpira utakwenda mbele.
Matumaini hayo pia yalitokana na hatua ya Makamu wa
Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad kuamua kwa makusudi kukutana na uongozi
mzima wa ZFA na wadau wa soka, wakati huo kabla kujiuzulu kwa Ali Ferej, na
kujadili kwa kina kinacholeta mivutano na kusaka muarobaini wa tatizo
hilo.
Wakati Wazanzibari wakianza kupata faraja na kuamini
kuwa sasa ni maendeleo tu na migogoro basi, ndani ya kipindi cha miezi saba tu
ya uongozi wa Amani Makungu, yameibuka makubwa na kumfanya Rais huyo aamue
kuomba kujiuzulu.
Ikitambua kwamba, kumkubalia Rais huyo aondoke, wengi
wataelewa kuwa huenda tatizo la ZFA liko ndani ya kamati zake tendaji Unguja na
Pemba, na pia katiba yake ambayo huko nyuma tuliambiwa eti imefanyiwa
marekebisho, ZFA ilichukua muda kumbembeleza Makungu afute uamuzi wake
huo.
Baada ya kuona maji yamezidi unga, na kwamba kila mmoja
sasa amefahamu kuwa chama hicho ni sawa na gunia la misumari lisiloweza
kubebeka, kwa shingo upande ZFA, ikiendelea kuvunja katiba kwa kufanya kikao cha
wajumbe wa kamati tendaji ya Unguja peke yao, iliridhia Makungu
aondoke.
Ni jambo lililozoeleka kwa chama hicho kimekuwa
kikifanya maamuzi mengi na mazito yanayokiuka katiba, ndivyo pia kilivyofanya
mara hii kwa kutoa baraka kwa Makungu kuachia ngazi, kwa kujikusanya kikundi tu
cha wajumbe wa Unguja na kuwasemea wenzao wa kisiwa cha Pemba katika jambo zito
kama hilo linalogusa maslahi ya taifa kimpira.
Hapa tu
panatosha kuipa nguvu serikali kuchukua maamuzi magumu ya kuivunja ZFA ambayo
imeonesha wazi kuwa inashindwa kuendesha mambo kwa mujibu wa katiba yake
iliyoiunda yenyewe.
Kama mtu mwengine yeyote aliyechoshwa na jambo, Makungu
alikuwa na haki ya kuomba kujiuzulu na hakukuwa na haja ya kumlazimisha
abakie.
Lakini pamoja na haki hiyo, je, ZFA huku ikiongozwa na
mwanasheria wake inayemtegemea, haikubaini kwamba kuamua bila kuwashirikisha
wenzao wa Pemba na kukubali ombi la Rais huyo, lilikuwa kosa?
Hapa ndipo
panapoibuka dhana kwamba kamati tendaji ya ZFA Unguja, inawatenga wenzao wa
upande wa pili kwani mara nyingi imekuwa ikifanya maamuzi makubwa peke
yake.
Yawezekana
kwamba huko Pemba nako wako wajumbe wanaoafiki Makungu kuachia ngazi, lakini si
kwa namna hii ilivyofanyika, ilipasa wote washirikishwe katika kutoa
uamuzi.
Je, madudu
haya yaliyofanywa na ZFA ambayo si mwanachama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa
(FIFA), hayatoshi kuionesha serikali kwamba sasa umefika wakati wa kufanya
maamuzi magumu na kukivunja chama hicho ili kuandaa mustakbali mzuri wa
baadae?
YAONEKANA hakuna
dawa mjarabu itakayokifanya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA)
kitawalike.
Kwa miaka mingi sasa, jitihada za serikali kuona soka
la Zanzibar linapiga hatua na kutambulika kimataifa, zimekuwa zikirudishwa nyuma
kutokana na migogoro isiyokwisha ndani ya ZFA.
Awali, kelele
za wadau zilikuwa zikielekezwa kwa viongozi wa chama hicho, wakidaiwa kuwa
hawana dhamira ya dhati kuiletea Zanzibar maendeleo katika mchezo wa mpira wa
miguu.
Kelele hizo zilimfanya Ali Ferej Tamim aliyekuwa Rais
wa chama hicho kwa zaidi ya miongo miwili, aamue kukaa pembeni na kuruhusu
kufanyika uchaguzi mdogo ili kupata Rais mwengine, ambaye alitarajiwa kushusha
presha za wadau waliokuwa wakililia mabadiliko.
Hatimaye,
Juni 30, mwaka jana, ZFA ikaitisha uchaguzi mdogo uliomuweka madarakani Amani
Ibrahim Makungu kuwa Rais kwa kipindi kilichobakia kabla ya uchaguzi mkuu wa
Disemba 2014.
Yalikuwa matumaini ya wengi, hata viongozi wakuu wa
Serikali ya Zanzibar ambao hawakusita kuelezea kuchoshwa kwao na migogoro ya ZFA
kila walipopata nafasi, kwamba sasa mpira utakwenda mbele.
Matumaini
hayo pia yalitokana na hatua ya Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif
Hamad kuamua kwa makusudi kukutana na uongozi mzima wa ZFA na wadau wa soka,
wakati huo kabla kujiuzulu kwa Ali Ferej, na kujadili kwa kina kinacholeta
mivutano na kusaka muarubaini wa tatizo hilo.
Wakati
Wazanzibari wakianza kupata faraja na kuamini kuwa sasa ni maendeleo tu na
migogoro basi, ndani ya kipindi cha miezi saba tu ya uongozi wa Amani Makungu,
yameibuka makubwa na kumfanya Rais huyo aamue kuomba kujiuzulu.
Ikitambua
kwamba, kumkubalia Rais huyo aondoke, wengi wataelewa kuwa huenda tatizo la ZFA
liko ndani ya kamati zake tendaji Unguja na Pemba, na pia katiba yake ambayo
huko nyuma tuliambiwa eti imefanyiwa marekebisho, ZFA ilichukua muda
kumbembeleza Makungu afute uamuzi wake huo.
Baada ya
kuona maji yamezidi unga, na kwamba kila mmoja sasa amefahamu kuwa chama hicho
ni sawa na gunia la misumari lisiloweza kubebeka, kwa shingo upande ZFA,
ikiendelea kuvunja katiba kwa kufanya kikao cha wajumbe wa kamati tendaji ya
Unguja peke yao, iliridhia Makungu aondoke.
Ni jambo
lililozoeleka kwa chama hicho kimekuwa kikifanya maamuzi mengi na mazito
yanayokiuka katiba, ndivyo pia kilivyofanya mara hii kwa kutoa baraka kwa
Makungu kuachia ngazi, kwa kujikusanya kikundi tu cha wajumbe wa Unguja na
kuwasemea wenzao wa kisiwa cha Pemba katika jambo zito kama hilo linalogusa
maslahi ya taifa kimpira.
Hapa tu panatosha kuipa nguvu serikali kuchukua maamuzi
magumu ya kuivunja ZFA ambayo imeonesha wazi kuwa inashindwa kuendesha mambo kwa
mujibu wa katiba yake iliyoiunda yenyewe.
Kama mtu mwengine yeyote aliyechoshwa na jambo, Makungu
alikuwa na haki ya kuomba kujiuzulu na hakukuwa na haja ya kumlazimisha
abakie.
Lakini pamoja na haki hiyo, je, ZFA huku ikiongozwa na
mwanasheria wake inayemtegemea, haikubaini kwamba kuamua bila kuwashirikisha
wenzao wa Pemba na kukubali ombi la Rais huyo, lilikuwa kosa?
Hapa ndipo
panapoibuka dhana kwamba kamati tendaji ya ZFA Unguja, inawatenga wenzao wa
upande wa pili kwani mara nyingi imekuwa ikifanya maamuzi makubwa peke
yake.
Yawezekana kwamba huko Pemba nako wako wajumbe
wanaoafiki Makungu kuachia ngazi, lakini si kwa namna hii ilivyofanyika, ilipasa
wote washirikishwe katika kutoa uamuzi.
Je, madudu
haya yaliyofanywa na ZFA ambayo si mwanachama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa
(FIFA), hayatoshi kuionesha serikali kwamba sasa umefika wakati wa kufanya
maamuzi magumu na kukivunja chama hicho ili kuandaa mustakbali mzuri wa
baadae?
No comments:
Post a Comment