BAADA ya
Arsene Wenger kuthibitisha kubaki Emirates inaelezwa kwamba amewaweka kwenye
rada zake mshambuliaji wa AC Milan kutoka Colombia, Carlos Bacca (30), winga wa
Leicester mzaliwa wa Algeria, Riyad Mahrez (26) na kiungo wa Monaco, Thomas
Lemar (21).
Wenger
inaelezwa anaruhusiwa kutumia pauni milioni 100 kwa ajili ya usajili, kiasi
ambacho bado ni kidogo, ikilinganishwa na Manchester City ambao wamemwambia Pep
Guardiola atumie hadi pauni milioni 250 kwa usajili. Liverpool na Man United
nao wanajipanga kuvunja benki, Chelsea wakisema hawana nia ya kutapanya fedha.
Mlinzi wa
Southampton, Virgil van Dijk (25) anapenda kujiunga Liverpool, wanaoelezwa
kwamba wapo tayari kumchukua Mholanzi huyo kwa pauni milioni 50 hivi ili
aimarishe kikosi chao tayari kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL).
Mshambuliaji
wa Ufaransa na Atletico Madrid, Antoine Griezmann (26) ameiambia klabu kwamba
anataka kuondoka, lakini kifungu cha mkataba cha kumwezesha kuaga Madrid
kinataka klabu chukuzi iweke mezani £87m, huku Manchester United wakihusishwa
na kumtaka.
Kiungo wa
Paris Saint-Germain (PSG) na Ufaransa, Blaise Matuidi (30) anasema kwamba hana
uhakika iwapo atakuwa klabuni hapo msimu ujao, na hizi ni habari njema kwa
United, kwani wamekuwa wakimtafuta kwa muda.
Jose
Mourinho anataka Matuidi acheze sambamba na Andre Herrera na pengine awe mrithi
wa Michael Carrick anayetarajia kuondoka Old Trafford baada ya mwaka mmoja. Pia
Matuidi anaweza kujiungisha vyema na Mfaransa mwenzake, Paul Pogba huko mbele.
Mlinzi
Mdachi wa Chelsea, Nathan Ake (22) anatarajiwa kuingia kwenye mazungumzo na
klabu kuona iwapo atahitajika klabuni au aende kwa mkopo msimu ujao.
Mshambuliaji
Mnigeria wa Manchester City, Kelechi Iheanacho (20) anataka kubaki England
japokuwa klabu wanaelekea hawampendi, na atakataa ofa kutoka kwa PSG ili
asubiri wengine wa England. Man City, hata hivyo, hawangependa kumuuza kwa
wapinzani wao katika EPL.
Kocha wa
Newcastle, Rafael Benitez anataka kuungana tena na kipa wa zamani wa Liverpool,
Pepe Reina na analenga kutoa pauni milioni nne kumchukua Mhispania mwenzake
huyo kutoka klabu ya Napoli, Italia.
Marseille wa
Ufaransa wanataka kumsajili winga wa Spurs, Moussa Sissoko wakati Chelsea
wanamtaka kipa wa PSG, Mfaransa Alphonse Areola (24) ili achukue nafasi ya raia
wa Bosnia, Asmir Begovic aliyejiunga na Bournemouth.
No comments:
Post a Comment