INGAWA Gor Mahia na AFC Leopards zinatoka Kenya, lakini kwa
matokeo ya leo ya fainali ya SportPesa, wimbo wa msanii wa Singeli Man Fongo ‘hainaga ushemeji tunakulaga,’ unawahusu.
Hiyo ni kutokana na mechi ya mahasimu hao kujulikana kama mechi ya
mashemeji kutokana na uhusiano wa timu hizo kutoka nchi jirani ambapo jana, Gor
Mahia ilidhihirisha haina cha ushemeji nyumbani wala ugenini baada ya kuifunga
Leopards mabao 3-0.
Matokeo hayo yamedhihirisha umwamba kwa Gor kwani ilipata ushindi
kama huo dhidi ya Leopards katika mechi ya Ligi Kuu Kenya mwezi uliopita.
Katika mechi ya jana, iliichukua mpaka dakika ya 60 kwa Gor
kuandika bao la kuongoza kupitia kwa Timoyh Otieno aliyefunga bao hilo kwa
shuti kali lililomshinda kipa wa Leopards Ian Otieno.
Dakika ya 72 Oliver Maloba aliongeza bao la pili kwa Gor baada ya
kupokea pasi nzuri ya George Odhiambo na kuujaza mpira wavuni.
Bao la tatu la mabingwa hao lilifungwa na John Ndorangu katika
dakika ya 90 kwa shuti kali akiunganisha pasi ya Odhiambo.
Ushindi huo unaifanya Gor Mahia kupata kitita cha dola za Marekani
30,000 (zaidi ya sh milioni 60) na Leopards ikivuna dola 10,000 (zaidi sh
milioni 20).
Timu nyingine zilizoshiriki michuano hiyo ni Simba, Yanga, Singida
United, Jang’ombe Boys na
Nakuru All Stars ambazo ziliishia njiani.
No comments:
Post a Comment