NAHODHA wa
Simba, Jonas Mkude ameruhusiwa kutoka hospitali alipokuwa amelazwa tangu juzi
baada ya kupata ajali ya gari eneo la Dumila mkoani Morogoro na ameshajiunga na kikosi cha Taifa Stars
Mkude
alikuwa amelazwa hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili, Dar es Salaam
kufuatia ajali baada ya gari walilikuwa wakisafiria kupasuka gurudumu moja na
kupinduka na kusababisha kifo cha Shose Fidelis.
Akizungumza
na gazeti hili Mkude alisema yuko vizuri na hana tatizo lolote ukiondoa
michubuko kidogo aliyopata.
“Daktari amesema nilipata mshituko tu baada ya ajali, lakini sijaumia popote na ninaweza kuendelea na kazi zangu kama kawaida,” alisema Mkude.
“Daktari amesema nilipata mshituko tu baada ya ajali, lakini sijaumia popote na ninaweza kuendelea na kazi zangu kama kawaida,” alisema Mkude.
Kabla ya
kuhamishiwa Muhimbili Mkude pamoja na majeruhi wengine walipata huduma ya
kwanza katika kituo cha afya Dumila na baadae kuhamishiwa hospitali ya mkoa wa
Morogoro.
Mkude alikuwa
anatoka Dodoma, ambako Jumamosi aliisaidia Simba kukata tiketi ya kucheza Kombe
la Shirikisho Afrika mwakani, baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC mchezo
uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Watu wengine
wawili waliokuwa katika gari hili Jasmin na Faudhia wamelazwa hospitali ya Mkoa
wa Morogoro na dereva ambaye pia ndiye mmiliki wa gari ajulikanaye kwa jina la
utani, Rais wa Kibamba anashikiliwa na Polisi.
Hii ni ajali
ya tatu kwa Mkude, alipata ajali Mbezi Dar
es Salaam lakini hakupata majeraha ya pili na ya tatu ni wakati anapelekwa Muhimbili
kwa matibabu zaidi gari yao ikamgonga mwendesha boda boda napo hakupata majeraha.
No comments:
Post a Comment