Liverpool
imepigwa Faini Pauni Laki 1 na kufungiwa kusaini Chipukizi baada ya
kukiri kuvunja Sheria za Ligi Kuu England, EPL, zinazolinda na kudhibiti
Usajili wa Makinda hao. Liverpool
wamepatikana na Hatia ya kumrubuni Chipukizi aliekuwa Klabuni Stoke
City na sasa hawaruhusiwi kusaini Chipukizi yeyote kwa Mwaka Mmoja na
Kifungo cha Mwaka Mmoja unaofuata kusimamishwa na kuwepo kwenye Angalizo
kwa Miaka Mitatu ili kosa hilo lisirudiwe.
Wasimamizi wa EPL wameridhika kuwa Liverpool ilijaribu kumrubuni Kijana wa Miaka 12 aliyesajiliwa na Stoke City kwa kutoa Ofa ya kumlipia Ada za Shule na kuwalipa Wazazi wake ili aihame kwao bila maridhiano kwa Klabu hizo mbili kitu ambacho kilikuwa kinyume cha taratibu.
EPL imesema Liverpool wamekiri Kosa lao na wamekubali Adhabu zao.

No comments:
Post a Comment