Harmorapa
si wa mchezo mchezo Usiku wa kuamkia leo Ameandika Historia Mpya ndani
ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, nazungumzia Dar Live uliopo Mbagala
Zakhiem baada ya kudondosha Bonge la Shoo tofauti n a watu walivyokuwa
wakimbeza. Harmorapa
ambaye anaonekana kuja kwa speed kali kwenye game ya Bongo Fleva
aliisimamisha Dar Live kwa takribani saa 1 kwa kupiga shoo kubwa kwa
mara ya kwanza Jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa Ujumla ambapo
alikuwa hajawahi kupata nafasi kama hiyo hapo awali. Harmorapa
aliwadhihirishia mashabiki wake kuwa yeye siyo wa kubeza kama baadhi ya
watu ambavyo wamekuwa wakimfikiria. Ngoma yake ya Kiboko ya Mabishoo
ilinyanyua mashabiki wote kwenye viti na kujikuta wakipagawa na kuivamia
steji huku kila mmoja akitaka kucheza ngoma hiyo na Rapa huyo. Shoo
yake ilikuwa ya kibabe huku akishangiliwa na umati mkubwa wa mashabiki
waliofurika Ukumbini hapo. Hakika ilikuwa ni Historia kwake na kwa
mashabiki wake kumtazama LIVE kwa mara ya kwanza aki-perform jukwaani
tena kwenye shoo kubwa kama ile. Katika
shoo hiyo, alikuwepo mkali wa Bongo Fleva, Juma Nature, Msaga Sumu na
wengine kibao ambao waliangusha burudani ya aina yake ukumbini hapo.
No comments:
Post a Comment