YANGA imerudi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu bara baada ya kuifunga Ruvu Shooting mabao 3-0 katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Ikicheza chini ya kocha wake mpya Mzambia George Lwandamina,
Yanga ilitawala vipindi vyote vya mchezo huo na kutoa burudani safi kwa
mashabiki wake waliofika uwanjani hapo.
Yanga iliandika bao la kuongoza katika dakika ya 38
baada ya mchezaji wa Ruvu kujifunga akiwa kwenye harakati za kuokoa mpira
uliopigwa na Simon Msuva.
Dakika ya 57, msuva aliandika bao la pili baada ya
kuunganisha pasi ya Deus Kaseke kabla ya kuongeza bao la tatu katika dakika ya
90 baada ya kuunganisha pasi ya Haruna Niyonzima.
Mechi ilikuwa ya upande mmoja zaidi kwa
Yanga kufanya mashambulizi langoni mwa Ruvu mara kwa mara ambapo katika dakika
ya 52 nusura Amisi Tambwe aandike bao baada ya kuachia shuti kali
lililopanguliwa na Hamisi Seif.
Dakika mbili baadae kocha Lwandamina anafanya
mabadiliko kwa kumtoa Tambwe na nafasi yake kuchukuliwa na Said Makapu.
Dakika ya 59 Ally Bilal alifanya shambulizi la nguvu
na nusura aipatia Ruvu bao lakini kutokuwa makini kulimfanya kupiga shuti
dhaifu lililodakwa na kipa wa Yanga Deogratius Munishi ‘Dida’.
Kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mwadui
ilishinda bao 1-0 dhidi ya Toto Africans na kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya
wenyeji Mbeya City walilazimishwa suluhu na Kagera huku Ruvu Shooting wakitoka
sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi.
No comments:
Post a Comment