Kwenye
mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya klabu hiyo yaliyopo mtaa wa Msimbazi
Kariakoo na kuhudhuriwa na wanachama 200 kutoka matawi 68.
Awali akizungumza
baada ya kufungua mkutano huo Rais wa Simba, Evans Aveva alisema mktano huo
utajadili ajenda mbili ambazo ni mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania na
mkutano mkuu wa dharura utakaofanyika Desemba 11.
“Ndugu
viongozi wenzangu nimewaita hapa ili tujadili mkutano mkuu unaotarajia
kufanyika Desemba 11 na mzunguko wa pili wa ligi kuu hivyo kabla ya kuanza
kujadili naomba wandishi wa habari watupishe ili tuweze kuendelea na mkutano
wetu,” alisema Aveva huku akishangiliwa kwa makofi.
Mkutano huo ambao
ulianza saa tisa alasiri uliohudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti, Geofrey Nyange
‘Kaburu’, Katibu Mkuu, Patrick Kahemele na wajumbe wa kamati ya Utendaji.
Awali Rais
wa Simba, Evans Aveva alisema Kamati ya Utendaji imeitisha mkutano mkuu wa
dharura unatarajiwa kufanyika Desemba 11, kwenye ukumbi wa Polisi Osyterbay Dar
es Salaam.
Hata hivyo
baraza la bodi ya wadhamini wa klabu hiyo chini ya Katibu wake Mkuu, Mzee Hamis
Kilomoni juzi aliitisha mkutano wa wandishi wa habari na kudai mkutano huo ni
batili na kumwomba mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuusimamisha.
VIONGOZI wa
Matawi wa klabu ya Simba leo wamefanya mkutano na kujadili ajenda mbili kuu.
No comments:
Post a Comment