Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limemteua Bi. Aziza Badru Mwanje kuwa Mkurugenzi mpya wa Fedha
na Utawala kuanzia Januari Mosi, 2017.
Uteuzi huo umefanywa leo (Desemba 17,
2017) na Kamati ya Utendaji ya TFF kufuatia mchakato wa usaili uliohusisha
waombaji wengine wawili na kufanywa na Bodi ya Ajira ya TFF.
Vilevile Kamati ya Utendaji imefanya
mabadiliko ya wajumbe katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ambapo Wakili
Patrick Sanga atakuwa Makamu Mwenyekiti wakati Mwenyekiti anaendelea kuwa
Wakili Richard Sinamtwa.
Wajumbe wengine walioongezwa kwenye
Kamati hiyo ni Bw. Adam Mihayo na Bw. Hassan Hassanoo ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA).
Wakili Raymond Wawa ameteuliwa kuwa
Mjumbe wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF kuziba nafasi ya Joseph
Mapunda ambaye ameomba kupumzika.
Pia Bibi Mia Mjengwa ameteuliwa kuwa
Mjumbe wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake.
No comments:
Post a Comment