Mlimbwende
anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17),
Anna Nitwa (wa pili kulia) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini
ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira,
Anthony Mavunde (wa pili kushoto) pamoja na madaktari wakati wakielekea
kwenye Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti),
katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.
Mrembo
huyo ambaye aliguswa na hali aliyoikuta hapo awali wakati alipotembelea
Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti) hasa pale
alipoona mazingira ya choo cha kina Mama hao kuwa si ya kuridhisha kwa
afya ya mama na Mtoto na ikizingatiwa kuwa watoto hao wanahitaji
uangalizi wa hali ya juu, alijitolea kukikarabati Choo hicho na Desemba
1, 2016 alikikabidhi kwa uongozi wa Hospitali hiyo ya Mkoa wa Dodoma.
Akizungumza
mbele ya wanahabari pamoja na uongozi wa Hospitali hiyo, Mrembo Anna
Nitwa alisema "Siku ya Novemba 4, 2016 nilitembelea Wodi ya Watoto Njiti
wakati wa kujiandaa na siku ya maadhimisho ya watoto wazaliwao kabla ya
wakati ambayo ilikua Novemba 17, Niliona mazingira ya choo kilichokua
kinatumiwa na Wazazi wa Watoto Njiti pamoja na wauguzi wao, hakikua
katika hali nzuri. Hivyo niliahidi kushirikiana na washikadau mbalimbali
ili kuweza kukarabati.
Aliendelea
kusema kuwa "Wazazi wangu pamoja na watu wachache walioguswa waliweza
kushirikiana nami kuchangia fedha za kukarabati choo hicho, na kazi ya
ukarabati imekamilika na sasa nimekikabidhi.
Kwa
Upande wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde
aliyeambatana na Mrembo huyo Hospitalini hapo, alimpongeza kwa kazi
nzuri aliyoifanya na kumuahidi kuijenga korido ambayo itaunganisha Wodi
hiyo na choo ili kuwasaidia wakina mama hao kuwa katika mazingira ya
ulinzi hasa nyakati za usiku, kwani kwasasa choo hicho kipo kwa nje ya
wodi hiyo, hivyo korido ikijengwa itawasaidia sana.
Kwa
upange wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Dodoma,Dkt. James Charles
alitoa shukrani kwa Mrombo huyo kwa jitihada zake za kufanikisha
ukarabati huo, na hasa kwa moyo wake wa kujitolea, na kuwaomba
Watanzania wengine kujitolea kufanikisha mahitaji mengine Hospitalini
hapo.
Mlimbwende
anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma
2016/17), Anna Nitwa (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Dodoma
Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na
Ajira, Anthony Mavunde (katikati) wakiwa katika Wodi ya Wazazi
wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa
wa Dodoma, Desemba 1, 2016.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma
Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na
Ajira, Anthony Mavunde akiangalia namna Choo hicho kilivyokarabatiwa kwa jitihada za Miss Dodoma
2016/17, Anna Nitwa.
Kinavyoonekana kwa ndani.
Mlimbwende
anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma
2016/17), Anna Nitwa akiwa amewabeba watoto Mapacha, wakati
alipotembelea Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati
(Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.
--
No comments:
Post a Comment