MWAMUZI wa soka wa kike wa
Kimataifa, Jonesia Rukyaa, amezawadiwa gari aina ya Toyota Vitz na Shirikisho
la Soka Tanzania, (TFF) baada ya kufanikiwa kuchezesha kwa mafanikio fainali za
Afrika za Wanawake.
Akizungumza wakati wa hafla ya
kumpongeza, Jonesia, Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema amefurahi kwa kiwango
ambacho Jonesia amekionesha hadi kufanikiwa kuchezesha mchezo wa mshindi wa
tatu kwenye faiinali hizo.
"Jonesia ameitangaza Tanzania
kwa kiwango ambacho amekionesha, sasa kamati ya waamuzi mnatakiwa mfanye kazi
ya kuwazalisha akina Jonesia wengi kutoka kwa wanaume na wanawake,"
alisema Malinzi
Pia Malinzi alisema ana imani
Jonesia atachezesha fainali zijazo za Afrika na fainali zijazo za dunia kwani
kwa sasa ni kati ya waamuzi bora watano barani Afrika kwa wanawake.
Malinzi alionesha kusikitishwa na
waamuzi Martin Saanya na Samwel Mpenzu kuondolewa kwenye ratiba ya Ligi Kuu na
kuitaka kamati kuchunguzza kwa makini na kutenda haki
Naye Jonesia Rukyaa aliwashukuru
wadau wote wa soka kwa michsango yao mbalimbali ambayo wamekuwa wakimpatia
kwani imemjenga na kumfanya kuwa bora na kutoa rai wanawake kuendelezwa kwnai
wanaweza.
"Kiukweli sikutarajia
kuchaguliwa kuchezesha fainali za wanawake barani Afrika kwani kwenye semina
nilikutana na waamuzi wenye uzoefu zaidi ya miaka kumi huku mimi nikiwa na
uzoefu wa miaka mitatu,|" alisema Jonesia
Pia aliishukuru TFF na Kamati ya
waamuzi kwa kumpanga kuchezesha mechi za wanawake hasa za Simba na Yanga kwani
zimemjenga na kumpa uzoefu.
Jonesia alichezesha mshindi wa tatu na
kupewa medali ya dhahabu anasema walianza wakiwa waamuzi 11 lakini walimaza
wakiwa nane tu kwa ilikuwa ukiharibu unaondolewa siku hiyohiyo.
Wakati huohuo, mchezo wa kirafiki wa
kimataifa wa timu ya soka la ufukweni dhidi ya Uganda unatarajiwa kuchezwwa leo
badala ya kesho kwenye Uwanja wa Karume, Dar ees Salaam.
No comments:
Post a Comment