Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara (VPL), mzunguko wa 15 unaomaliza duru la kwanza kwa msimu
huu, inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa timu 12 kuchuana kwenye viwanja
sita.
Kwa keshotwa Jumapili,
African Lyon inatarajiwa kucheza na Simba kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam
katika mchezo Na. 144 wakati Mbao itakuwa mwenyeji wa Azam FC Uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza katika mchezo Na. 116.
Kwa upande
wake, Ndanda siku ya Jumapili itakuwa mwenyeji wa Stand United ya Shinyanga
kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara kwenye mchezo Na 117 wakati
Tanzania Prisons inatarajiwa kuialika Young Africans kwenye Uwanja wa Sokoine
jijini Mbeya katika mchezo Na. 118.
Kagera Sugar
kwa upande wake siku hiyo ya Jumapili itacheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja
wa Kaitaba mjini Bukoba, mjini Kagera katika mchezo ulipewa Na. 119 ilihali JKT
Ruvu itakuwa mwenyeji wa Toto Africans kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko
Mlandizi mkoani Pwani kwenye mchezo Na. 120.
Ligi hiyo
itaendelea Jumatatu kwa michezo miwili ambako Mtibwa Sugar itaialika Mbeya City
kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Morogoro katika mchezo Na. 113 wakati Mwadui
itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Mwadui huko Shinyanga
katika mchezo ulipewa Na. 115.
No comments:
Post a Comment