TIMU ya Soka
ya wanawake, JKT Queens imefunga timu ya Viva ya Tanga mabao 12-2 kwenye mchezo
wa Ligi Kuuya Wanawake uliochezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam juzi.
Mchezo huo
ambao ulikuwa wa upande mmoja ulihudia JKT Queens wakienda mapumziko wakiwa
mbele kwa mabao 6-0 na kipindi cha pili walifunga mabao sita mengine na Viva
wakafunga mabao mawili.
Shujaa wa
mchezo huo alikuwani mshambuliaji wa JKT Queens, Fatuma Swalehe ambaye alifunga
mabao sita peke yake, akifuatiwa na Asha Rashid 'Mwalala na Zena Rashid ambao
kila mmoja alifunga mabao mawili
Karamu ya
mabao ilihitimishwa na Marry Masatu na Anna Hebron ambao kila mmoja alitupia
nyavuni bao moja moja.
Mabao ya
Viva yalifungwa na Aisha Shaban kwa njia ya penalti baada ya yeye mwenyewe
kufanyiwa faulo na beki wa JKT Queens, Happy Mwaipaja na lingine likafungwa na
Mgeni Ramadhan.
Akizungumza
baada ya mchezo, kocha wa JKT Queens, Robert Ngoliga alisema dhamira yao ni
kuchukua ubingwa na ndio maana wachezaji wake wanajitahidi kuufunga mabao mengi
iwezekanavyo.
"Dhamira
yetu ni ubingwa na ndio maana tumefanya usajili wa uhakika na kila mechi
tunahesabu kama ni fainali kwetu," alisema Ngoliga.
Timu ya JKT
Queens inaundwa na wachezaji ambao asilimia kubwa wanacheza timu ya Taifa ya
wanawake 'Twaiga Stars'
No comments:
Post a Comment