TIMU ya Soka
ya wanawake, JKT Queens imefunga timu ya Viva ya Mtwara mabao 12-0 kwenye
mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliochezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam jana.
Mchezo huo
ambao ulikuwa wa upande mmoja ulihudia JKT Queens wakienda mapumziko wakiwa mbele
kwa mabao 4-0 na kipindi cha pili walifunga mabao nane mengine.
Shujaa wa
mchezo huo alikuwani mshambuliaji wa JKT Queens, Asha Rashid 'Mwalala' ambaye
alifunga mabao sita akifuatiwa na Donesia Anthony ambaye alifunga mabao matano
na Johari Hamis ambaye alihitimisha karamu kwa kufunga bao moja.
Dakika ya 80
Kipa wa Viva, Zuhura Abdallah aliumia baada ya kugongana na nahodha wa JKT
Queens wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa mpira kwenye eneo lake na
kulamika kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Amana kwa uchunguzi zaidi.
Zuhura alipigwa teke la tumboni hali
iliyomsababishia maumivu makali na kushindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake
kuchukuliwa na Husna Kombo.
Akizungumza
baada ya mchezo, kocha wa JKT Queens, Robert Ngoliga alisema dhamira yao ni
kuchukua ubingwa na ndio maana wachezaji wake wanajitahidi kuufunga mabao mengi
iwezekanavyo.
"Dhamira
yetu ni ubingwa na ndio maana tumefanya usajili wa uhakika na kila mechi
tunahesabu kama ni fainali kwetu," alisema Ngoliga.
Kwenye
mchezo mwingine uliochezwa Uwanja wa Samora Iringa, Panama iliifunga Baobab bao
1-0.
No comments:
Post a Comment