SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF), limesema haitambui mababiliko ya uendeshwaji wa Klabu
ya Yanga; badala yake wameuandikia uongozi wa Yanga barua wakitaka nakala ya
mkataba wa ukodishwaji wa klabu hiyo kwa miaka kumi kwa mwekezaji
anayetambulishwa Yanga Yetu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine alisema
kwamba TFF imekuwa ikipokea barua kutoka kwa wadau mbalimbali wa Yanga wakihoji
taratibu au hatua zinazoendelea katika mfumo wa umiliki na uendeshwaji wa timu
hiyo.
Mbali
ya hatua hiyo, Alhamisi iliyopita ya Oktoba 6, 2016 vyombo mbalimbali vya
habari (si HabariLeo) vilikuwa na taarifa kuhusu muhtasari wa mkataba wa Yanga
wa kukodishwa na kampuni ijulikanayo kama Yanga Yetu Limited.
“Simba
na Yanga wamekuja na mabadiliko ya kutaka kubadili mfumo wa uendeshaji na
tukaziandikia kutaka kukutana nazo kutaka kujua uhalisia na Simba walikubali,
lakini Kaimu Katibu Mkuu aliwajibu na kuwataka wawasiliane na wajumbe wa Baraza
la Udhamini ndiyo wenye majibu juu ya mchakato wa ukodishwaji,” alisema
Mwesigwa.
“Baadaye
tunasikia kwenye magazeti kuwa kuna kampuni moja ambayo wamesaini nayo
mkataba... Ndipo tukashtuka hivyo tunataka kujua status (hadhi) ya mkataba. Je,
huo mkataba una husu timu A tu na programu za vijana itakuweje ndio vitu
tunataka kujua japo klabu hiyo imesajiliwa kikatiba,” alisema Mwesigwa.
Kadhalika,
Mwesigwa amesema wanataka kuona kilichopo kwenye mkataba kabla ya kushauri ili
kuangalia kama vinakwenda sambamba na matakwa ya TFF, CAF na FIFA ili kuondoa
malalamiko ambayo yamekuwa yakiendelea kwani wengine wamefika hatua ya kuomba
idhini ya TFF kwenda kumwona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John
Pombe Magufuli.
Mwesigwa
alisema wanataka kujua pia nani anamiliki na nani anaendesha timu na umiliki
wake ukoje kwa maana hizi timu za Simba na Yanga zinagusa nyoyo za watu wengi
na taratubu za uhamishaji umiliki wake ukawa wa wazi-hadharani.
“Mambo
ya kubadilisha uendeshwaji unatakiwa kufuata taratibu ikiwa ni pamoja kuenenda
sawa na katiba ya klabu, kamati ya utendaji ifahamu, mkutano mkuu uridhie ili
kujua nini kinauzwa na nini kinakodishwa ikiwa ni kwenye level (hatua) ya
klabu.
“Kama
itakuwa nje ya utaratibu wetu wa uendeshaji wa klabu kamati ya sheria na kamati
ya utendaji watafanya kazi na kama watakuwa wamefuata taratibu inaweza isifike
huko kwenye CAF na FIFA,” alisisitiza Mwesigwa.
Mwesigwa
alisema TFF itaendelea kuwasiliana na Kaimu Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit au
Mwenyekiti, Yussuf Manji kwa mambo yote yanayohusu sera na mipango na siyo Bodi
ya Wadhamini kama ambavyo Baraka alielekeza.
Pia
Mwesigwa amesema hawaangalii tu mtu anayekodisha ana pesa kiasi gani bali hata
kamapuni hiyo inatoka nchi gani na mmiliki ana historia gani huku amkimtolea
mfano Roman Abromovich alipokwenda kununua Chelsea.
“Msimamo
wa TFF ni kwamba klabu ya Yanga ipo kama ilivyokuwa kwa mujibu wa
taratibu za TFF, CAF na FIFA hadi hapo watakapo pata barua toka Yanga na
wanatambua uongozi wa Mwenyekiti Yussuf Manji na Kaimu katibu Mkuu Deusdedit
Baraka.
No comments:
Post a Comment